12th May, 2021
Chama cha Jubilee kinaendelea kiwaadhibu waasi chamani haswa wandani wa Naibu Rais William Ruto bungeni. Kamati ya kitaifa ya usimazi sasa ikielekeza mjeledi kwa mbunge wa Gatundu Moses Kuria na mbunge maalum Cecily Mbarire ambao sasa wanakodolea macho kubanduliwa chamani. Hii inajiri tayari Isaac Mwaura akiwa amepoteza nafasi yake ya useneta.