.
8th May, 2021
Usiku wa leo, maafisa wa polisi wanadai kuwa wamefanikiwa kumtambua mwanamme mshukiwa mkuu kwenye mauaji ya aliyekuwa meneja wa mawasiliano katika tume ya ardhi Jennifer Wambua kupitia uchunguzi ambao umekuwa ukiendelea. Mshukiwa huyo Peter Mwangi Njenga amekuwa korokoroni kwa takriban siku thelathini wakati uchunguzi ukiendelea.