.
22nd April, 2021
Shughuli ya kurekebisha katiba kupitia mchakato wa BBI imegubikwa na usiri na malumbano kuhusu mapendekezo kadhaa. Tofauti na utaratibu mwigine wa kurekebisha katiba kama ilivyokuwa wakati wa bomas hadi katiba ya 2010 ambapo serikali ilihakikisha wananchi wanapata nakala zote na kujifahamisha yaliyomo, mambo yamekuwa tofauti na mswada wa BBI. Tume ya uchaguzi iliwasilisha nakala ya bbi kwa mpiga chapa wa serikali ili kuwasilishwa kwa kaunti zote 47. Je, nini kilichojiri kwenye afisi za mpiga chapa wa serikali ndipo miswada miwili kinzani ikachapishwa na kuwasilishwa kwa mabunge ya kaunti?