21st April, 2021
Aliyekuwa OCS wa Makuyuni, kaunti ya Makueni amefikishwa mahakamani leo kwa madai ya kuchukua rushwa ya shilingi elfu tano na matumizi mabaya ya ofisi. Henry Mutunga anadaiwa kumtia mbaroni mhudumu mmoja wa bodaboda na kumwitisha shilingi elfu kumi ili kumwaachilia huru baada ya jamaa huyo kukiuka kanuni za kafyu.