20th April, 2021
Saa chache za mahangaiko kwa mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari ya wasichana ya St. Georges Grasslands katika kaunti ya Nakuru zimekamilika mapema leo hii baada ya kupata fursa ya kuelekea nyumbani kwao likoni, kaunti ya Mombasa. Mwanafunzi huyo aliyekamilisha mtihani wake wa kidato cha nne (KCSE) hapo jana, alidaiwa kuzuiliwa na usimamizi wa shule iyo kuondoka baada ya wazazi wake kukosa kukamilisha deni la karo ya shilingi elfu tisa. Ilimlazimu binti huyo kutoroka shuleni na kutafuta pa kulala kutoka kwa wasamaria wema kabla ya kupata njia ya kusafiri, lakini anavyoarifu mwanahabari wetu Ibrahim Karanja usimamizi wa shule hiyo umekataa kata kata kwamba ulimzuia mwanafunzi huyo kuondoka shuleni.