.
15th April, 2021
Na baada ya matokeo hayo kutangazwa, baadhi ya shule zilizofanya vyema zilianza kusherehekea matokeo mazuri ya mtihani wa darasa la nane KCPE. Wanafunzi, walimu na wazazi katika baadhi ya shule maeneo mbalimbali ya nchi walifurahia kwa nyimbo, huku wengine wakimshukuru mungu kwa matokeo mema. Idadi kuu ya wanafunzi waliopokea matokeo mazuri walimiminika katika shule zao kukutana na walimu wao. Wengi walikua na matarajio ya kuendelea na masomo ya shule ya upili, baada ya jitihada zao kuzaa matunda.