.
14th April, 2021
kwa mara nyingine tena, familia ya aliyekua rais wa marekani Barack Obama, inaomboleza kuondokewa na mamake wa kambo keziah aoko ontango aliyefariki katika hospitali moja mjini london uingereza. Nduguye wa kambo malik obama alithibitisha kifo hicho huku akiitaka serikali ya kenya kusaidia kuusafirisha mwili wake hadi humu nchini kwa mazishi. kifo cha mama keziah ambaye amekua akiishi uingereza kwa zaidi ya miaka 10 kinakuja wiki chache baada ya kifo cha nyanyake obama, sarah obama. marehemu keziah aliyekua na umri wa miaka 78 ameacha watoto 4 akiwemo malik, auma, abuu na sadique.