.
14th April, 2021
Tume ya uchaguzi na mipaka IEBC huenda ikalazimika kuweka mitambo ya kupeperusha na kuhifadhi matokeo ya uchaguzi almaarufu servers nchini iwapo mapendekezo yanayotolewa na wizara ya ICT yatatimizwa. wizara hio iko katika harakati za kubuni sheria zaitakazosaidia kutekeleza sheria za kuchunga na kutunza taarifa muhimu yaani data zilizotiwa sahihi na rais kenyatta. katika mapendekezo haya kila mitambo inayotumika kuhifadhi tarifa zozote sharti iwe humu nchini, ikiwemo mitambo ya kupeperusha matokeo ya uchaguzi nchini. daniel kariuki anaarifu.