Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan atangaza mikakati mpya ya kupambana na virusi vya Korona
07, Apr 2021
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametangaza nia ya serikali yake kushirikiana na ulimwengu katika harakati za mapambano dhidi ya virusi vya korona. Kauli hiyo ya Rais Samia inasahihisha alichokiamini mtangulizi wake dkt. John Pombe Magufuli, ambaye hadi umauti unamkuta march 17 mwaka huu, aliamini korona inazuilika kwa maombi na kujifukiza mvuke wa dawa asili za mitishamba.