7th April, 2021
Mwanaharakati Edwin Kiama atazuiliwa katika kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi huku akisubiri uamuzi kuhusu dhamana. Kiama alikamatwa siku ya Jumanne kwa madai ya matumizi ya mtandao. Amefika mbele ya Hakimu Jane Kamau ambaye atatoa uamuzi kuhusu dhamana siku ya Alhamisi saa tatu asubuhi.