.
1st March, 2021
Shule moja ya msingi iliyopo katika kijiji cha kudema mkoani Singida nchini Tanzania, ina mazingira duni ya kujifunzia, ambapo wanafunzi wa shule hiyo huketi chini ndani ya darasa dogo, lililojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi. Shule hiyo inagundulika ikiwa na mazingira magumu, licha ya taifa hilo kuwa na mipango mbalimbali ya maboresho ya elimu kwa ngazi zote.