.
26th February, 2021
Huenda waakilishi wadi wakatozwa kodi ya asilimia thelathini kwenye ruzuku ya shilingi milioni mbili wanayotarajia kupokea ya kununua magari. Kwenye barua aliyoandikiwa mwenyekiti wa baraza la magavana, Martin Wambora, na kamishena wa ushuru wa mapato ya ndani katika mamlaka ya mapato nchini, kra, risper simiyu, ruzuku hiyo imeorodheshwa kuwa mapato, hivyo basi KRA imesema kwamba iwapo waakilishi wadi watapokea fedha hizo, ni lazima watozwe kodi