22nd February, 2021
Watoto kutoka familia zisizojimudu katika kituo cha watoto cha wamo huko kawangware eneo la gatina walipata ugeni wa aina yake kutoka kwa wahisani waliojumuika nao kwa mlo.Wahisani hao wakiongozwa na ajay jawla waliwaandalia watoto hao mlo na kuwapa matumaini maishani kwamba jamii haijawatelekeza. Msimamizi wa kituo hicho kennedy swaka aliwashukuru kwa hatua hiyo na kuwarai wakenya wanaojiweza kuwajali watoto wasiobahatika. Kituo hicho kina watoto wapatao mia tatu.