9th February, 2021
Na huku Kisumu wakipiisha mswada huo, mabunge mingine ya kaunti yamerejelea vikao vyao hii leo huku mswaada wa marekebisho ya katiba kupitia BBI, ukiwa miongoni mwa ajenda kuu. Mswaada huo tayari umewasilishwa rasmi na kuelekezwa kwa kamati husika huku shughuli ya kuihusisha umma ikipangwa katika baadhi za kaunti. Pia, wawakilishi wadi wa kaunti ya Baringo wameitwa kikao na usimamizi wa Jubilee, kabla kuanza kusikiza mswada huo.