.
26th January, 2021
Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amewataka vijana kuunga mkono BBI na kusema kwamba ndiyo itakayowafungulia milango ya ufanisi. Odinga aliyekuwa ameandamana na wanachama wengine wa ODM, alikutana na viongozi wa vyama vya wanafunzi wa vyuo vikuu, kuso, ajenda ikiwa ni kuipigia debe BBI.