24th January, 2021
Seneta wa Baringo Gideon Moi amewahakikishia wakazi wa mogotio kaunti ya baringo kuwa miradi iliosimama ya ujenzi wa barabara itaedelea karibuni. Akizungumza katika kijiji cha mugurin sehemu ya mogotio kaunti ya Baringo, Moi alisema kuwa bajeti ya ujenzi wa barabara ya kamukunji kisana na kipkitur mugurin hadi ziwa Bogoria tayari imepitishwa. Alizungumza na wakazi baada ya kuhudhuria ibada katika kanisa la aic mugurin. Wakazi wa eneo hilo awali walimtaka gideon kuwasaidia kutamatisha miradi iliyoahidiwa na serikali zikiwemo barabara zilizokwama kwa zaidi ya miaka mitatu pamoja na tatizo la ukosefu wa maji.