Charity Ngilu apinga madai ya Ruto kwamba Kalonzo Musyoka alinyakua ardhi ya NYS eneo la Yatta
19, Jan 2021
Kiongozi wa chama cha wiper Kalonzo Musyoka sasa anamtaka naibu Rais William Ruto kukubali wafanyiwe uchunguzi wa kina na wazi kuhusu mali wanayomiliki hususan masuala ya mashamba baada ya ruto kudai kwamba musyoka amejenga makazi yake huko yata kwenye ardhi aliyonyakuwa. Akijibu madai hayo, kalonzo anashinikiza kwamba ruto akubali kufanyiwa uchunguzi wa angalau sakata saba za ardhi miongoni mwa sakata zingine anazohusishwa nazo.