.
14th January, 2021
Wakazi wa mtaa wa mabanda wa Motherland ulioko Eastleigh jijini Nairobi sasa wanahofia afya yao baada ya taka na maji kuingia hadi majumbani mwao wasiwe na pa kukimbilia. Mwanahabari Sycilia Wakesho Mathuva aliyezuru mtaa huo anaripoti kwamba wakazi wanalaumu mvutano kuhusiana na uongozi wa nairobi kuwa chanzo cha masaibu yao.