13th January, 2021
Huku kenya ikitarajiwa kuwa na kibarua kigumu katika michuano ya kufuzu kwa kipute cha bara afrika dhidi ya Misri na Togo, Victor Wanyama nahodha wa Harambee Stars ana imani kuwa Kenya itakuwa na matokeo mema mwaka 2021. Aidha ameangazia msimu wake ligi ya marekani na uhusiano wake na kocha Thierry Henry.