27th December, 2020
Mwenyekiti wa baraza la magavana na gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya amesema wamekubaliana na serikali kuu kujenga kituo cha kwanza cha saratani kuwahudumia wakaazi wa eneo la magharibi. Hatua hii ni kutokana na saratani kuwa miongoni mwa magonjwa yanayowaathiri wakaazi wa magharibi kwa wingi. Magavana wote wa kaunti zote za magharibi wangali wanajadiliana ni katika kaunti ipi kituo hicho kitajengwa na kuwa rahisi kwa wagonjwa kusafiri kutoka maeneo mbali mbali ya magharibi.