.
9th December, 2020
Ulimwengu unapoadhimisha siku ya kukabili ufisadi, tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC, imesema imefanikiwa kurejesha takriban shilingi bilioni 6.1 zilizoporwa mwaka huu. Akizungumza katika sherehe za leo zilizoandaliwa katika kaunti ya kiambu, mwenyekiti wa Eacc Eliud Wabukala, amewakumbusha wakenya kuwa vita vivyo ni vya wakenya wote na kila mmoja awajibike kuwaanika mafisadi nchini.