×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Mustafa Idd amefariki: Alikuwa mbunge wa Kilifi kusini, amezikwa leo nyumbani kwao Bomani

25th November, 2020

Aliyekuwa mbunge wa Kilifi Kusini Mustafa Iddi ambaye aliaga dunia ghafla mapema hivi leo akifanyiwa matibabu katika hospitali ya Premier Mjini Mombasa amezikwa nyumbani kwao eneo la Bomani kaunti ya Kilifi. Kwa mujibu wa familia yake, Mustafa ambaye alikuwa mwanahabari wa siku nyingi kabla ya kujiunga na siasa alipata matatizo ya kupumua kutokana na ugonjwa wa pumu na kisha kukimbizwa hospitalini ambako aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 50. Atakumbukwa kwa kuwa mwandishi wa habari katika shirika la habari nchini KBC alikoanzia taaluma yake ya uanahabari kabla ya kujiunga na Runinga ya NTV. Alijiunga na siasa kwa mara ya kwanza mwaka 2007 ambapo aligombea kiti cha eneo bunge la Bahari bila kufanikiwa.  Baadaye alichaguliwa kuwa bunge wa eneo la Kilifi Kusini kwa tiketi ya chama cha ODM mwaka 2007 lakini akapoteza kiti hicho mwaka 2017 akigombea kwa tiketi ya chama cha Jubilee. Hadi kifo chake alikuwa akihudumu kama mwenyekiti wa Shirika la maendeleo ya miradi ya maji ukanda wa Pwani.

.
RELATED VIDEOS