Mzozo wa Jaa la Taka: Viongozi katika eneo la Embakasi wakutana na vijana Kayole
18, Nov 2020
Viongozi eneo la Embakasi ya kati wamefanya mkutano na vijana wa kuokota taka eneo la kayole ili kutatua mzozo uliokuwepo kuhusu ni wapi taka hiyo inafaa kutupwa. Hapo awali, mamlaka ya usimamizi wa jiji la nairobi NMS ilikuwa imewasimamisha vijana dhidi ya kazi hiyo ya kuokota taka jambo lililokuwa limeanza kuleta hali ya wasiwasi miongoni mwa vijana wengi wanaotegemea kazi hiyo kujikimu kimaisha.