x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Mbaka ahojiwa na EACC kuhusu tukio la hivi juzi ambapo alidhalilishwa na Waziri Magoha

18, Nov 2020

Mkurugenzi wa Elimu katika Kaunti ya Uasin Gishu Mbaka Gitonga ambaye alisemekana kudahlilishwa na Waziri wa Elimu Prof George Magoha alipozuru kaunti hiyo wiki mbili zilizopita amehojiwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi EACC. Mbaka ametakiwa kuandikisha taarifa kuelezea kilichojiri na kumsababisha Waziri Magoha kumtukana hadharani. EACC imethibitisha kuwa uchunguzi unaendelea kuhusiana na tukio hilo. Wiki mbili zilizopita waziri magoha alipozuru Shule ya Msingi ya Langas mjini Eldoret alinaswa kwenye video akitumia maneno ya matusi dhidi ya Mbaka Gitonga kisa ambacho kilikashifiwa vikali.

Feedback