.
18th November, 2020
Majukumu na matarajio katika jamii yamekuwa chanzo cha madhara kwa wengi haswa magonjwa ya kiakili miongoni mwa wanaume. Mara nyingi wengi hawapendi kuzungumza na hili limesababisha ongezeko la visa vya matatizo ya kiakili na wengine kujitia kitanzi miongoni mwa jinsia ya kiume. Kenya itakapojumuika na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya wanaume hapo kesho ni mengi tu ambayo taifa la Kenya lafaa kuangazia kuu likiwa suala la Afya kwa wanaume.