.
18th November, 2020
Wabunge sasa wanataka kuwe na ndege ya dharura kila wakati ili kuwasafirisha kwa matibabu wanaolemewa na makali ya korona. Haya yanajiri siku chache baada ya mbunge wa Matungu Justus Murunga kufariki baada ya kukosa mitambo ya hewa ya oksijeni kwenye hospitali iliyokuwa karibu. Hayo yakiarifiwa, wahudumu wa afya kutoka kaunti nyingi nchini wamezidi kuelezea mafadhaiko yao na hali katika sekta ya afya nchini. Viongozi wa wahudumu wao chini ya muungano wa KMPDU walifika mbele ya kamati ya bunge ya afya kuelezea masikitiko yao.