11th November, 2020
Tume ya kitaifa ya Uwiano na utangamano NCIC inaendelea kuweka mikakati zaidi ya kuhakikisha wanasiasa watakao toa cheche za maneno wanakabiliwa kwa mjibu wa sheria. Kamishna wa tume hiyo Wambui Nyutu amesema kwamba maafisa wa NCIC watatumwa kuhudhuria mikutano yoyote ya kisiasa ambayo itakuwa sehemu mbalimbali kusikia na kunakili maudhui yake. Akizungumza jijini Mombasa wakati wa kongamano la kuwahamasisha maafisa wa polisi na waongoza mashtaka namna ya kutambua na kushughulikia washukiwa wa matamshi hayo, Nyutu vilevile amesema kwamba tayari maafisa wa polisi kote nchini wamesambaziwa kamera za siri ambazo pia zitatumiwa kufanikisha lengo hilo.