Uchungu wa Familia: Mama awapoteza wanawe kwa Al-Shabaab, watoto wake walijiunga na kundi
11, Nov 2020
Mama mmoja katika kaunti ya Mombasa anaendelea kusononeka baada ya wanawe wanne kati ya kumi na mmoja kuhusishwa na kundi la kigaidi la Al shabaab. Mmoja wa wanawe aliuawa, wapili yuko jela ya shimo la tewa, watatu ambaye ni wa kike akisemekana aliozwa kwa mwanamgambo wa Al shabaab nchini Somalia na ambaye alifariki huku wanne akiwa ametoweka nyumbani kwao mwezi jana na hadi wa leo hajulikani aliko.