8th November, 2020
Watu wanaosihi na ulemavu katika kaunti ya Taita Taveta wameonyesha kuridhika kwao na hatua ya chama cha ODM kubuni kundi maalum la walemavu maarufu kama 'Odm Disabled League' wakisema itasaidia kuhakikisha wanatwaa nafasi muhimu za uongozi siku za mbeleni. Waakilishi wao taita taveta wamehakikisha kuwa watafuata msimamo wa chama cha ODM kuunga mkono ripoti ya upatanishi nchini BBI.