.
8th November, 2020
Wataalam wa masuala ya watoto wanaonya kwamba huenda watoto wakaathirika zaidi kutokana na makali ya janga la korona. Onyo hili linafuatia hali kwamba zaidi ya watoto milioni kumi wanaostahili kuwa shuleni watalazimika kuwa nyumbani kwa miezi mingine miwili zaidi kufuatia tishio la virusi vya korona. Hata hivyo muungano wa mataifa ya ulaya, EU, umetangaza ufadhili wa mradi maalum utakaoyahusisha mashirika mbalimbali kwa lengo la kuwaokoa watoto dhidi ya dhuluma na mateso mengine kwenye majira haya ya Covid?19.