Ukuzaji Vipaji: Timu kutoka Murang'a na Kiambu kunufaika, zaidi ya vilabu 140 wapokea sare
08, Nov 2020
Zaidi ya timu 140 kutoka kaunti ya Muranga na Kiambu hii leo zilipigwa jeki baada ya kupokea vifaa vya kucheza kutoka kwa kampuni ya odibets ikishirikiana na shirikisho la kandanda nchini fkf. Timu hizo ambazo pia zinashiriki ligi ya kaunti zilipokea sare za kucheza kwa maandalizi ya msimu mpya.