.
2nd November, 2020
Bingwa wa dunia wa mbio za mita elfu moja mia tano Timothy Cheruiyot ameteuliwa kuwania taji la mwanariadha bora duniani upande wa wanaume. Cheruiyot aliandikisha mda bora msimu huu wa dakika tatu sekunde 28.45. Vile vile cheruiyot hakupoteza mbio za elfu tano alizoshiriki msimuhuu. Bingwa huyo atawania taji hilo pamoja na wanariadha wenginge tisa akiwemo mshikilizi wa rekodi ya mita elfu tano na elfu kumi Joshua Cheptegei kutoka Uganda na Donovan Brazier kutoka Marekani.