1st November, 2020
Utata unazidi kuzingira kifo cha msichana wa umri wa miaka kumi na sita aliyepatikana ndani ya kisima kimoja eneo la kihuho, kaunti ya kiambu kilomita takriban nne kutoka nyumbani kwao. Mercy Wanjiru Mwangi anadaiwa kupotea tarehe kumi na tisa mwezi jana kabla ya kupatikana siku tatu baadaye. Licha ya ripoti ya polisi kusema kuwa binti huyo alijitia kitanzi familia inataka uchunguzi zaidi kubaini kiini cha kifo hicho