x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Viongozi walifungua roho zao katika Ukumbi wa Bomas, walielezana ukweli wa mambo

26, Oct 2020

Rais Uhuru Kenyatta ameshikilia kuwa ripoti ya BBI itajumuisha watu wote na hailengi kuwatupa nje baadhi ya viongozi. Rais amesema safari hii inafaa kuwajumuisha wote ili iweze kuleta manufaa yanayofaa. Kiongozi wa ODM Raila Odinga amesisitiza kuwa Ripoti ya BBI inalenga kuleta amani ya kudumu nchini ambayo imekuwa ikitikiswa kila wakati haswa kutokana na tofauti kali za kisiasa. Odinga ameshikilia kuwa, ripoti hii sio ya kuwanufaisha baadhi ya wakenya na kuwakandamiza wengine. Naibu wa Rais William Ruto amesisitiza ufafanuzi zaidi kuhusu nyadhifa za juu zinazoashiriwa na Ripoti ya BBI, akisema kuwa mwanga zaidi unafaa kutolewa kuhusu jinsi nafasi hizo zitakavyozika kwenye kaburi la sahau malumbano ya kisiasa ambayo yamekuwa wakishuhudiwa humu nchini. Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanya kazi nchini COTU Francis Atwoli ameshinikiza katiba kutoa nafasi ya uwakilishi wa wafanyakazi bungeni bila kupitia kwenye vyama vya kisiasa. Amesema kuwa BBI itasaidia pakubwa kuleta amani nchini, kwani ghasia ambazo hushuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu huathiri sana wafanyakazi wengi. 

Feedback