21st October, 2020
Kumekuwa na hisia kinzani saa chache tu baada ya ripoti ya maridhiano ya bbi kukabidhiwa Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa Odm Raila Odinga. Mrengo unaomuunga Naibu wa Rais William Ruto umekariri kwamba, utapinga mchakato huo, ikiwa utakuwa wa kuwapa vyeo baadhi ya vigogo nchini. Wakenya mitaani pia walilivalia njuga swali hilo.