20th October, 2020
Wanafunzi wa gredi ya nne na darasa la nane, wataanza mitihani yao hapo kesho ili kubaini uthabiti wa kumbukumbu zao baada ya kuwa nyumbani kwa miezi sita. Baraza la mitihani nchini, knec, limeitaja mitihani hiyo kuwa mijarabu ya kupima na kubaini utayari wa wanafunzi kuendelea na masomo baada ya kuwa nyumbani kwa kipindi kirefu. Ila anavyoripoti Shadrack Mitty, shule nyingi zinakabiliwa na chanagamoto za kupata karatasi za mitihani kutoka wavuti wa KNEC.