14th October, 2020
Seneta wa Baringo Gideon Moi hii leo alijiunga na nduguye john mark moi na familia yake kwenye mazishi ya mama mkwe wa John Mark, Elma Kabon Tunai katika eneo la Rongai kaunti ya Nakuru. Seneta Gideon alimtaja mama elma kama mama mcha mungu aliyewaleta wengi pamoja. Elma Kabon Kenchwel alizaliwa mwaka wa elfu moja mia kenda thelathini na sita katika kijiji cha Ketigor, kaunti ya Elgeyo Marakwet. Viongozi kadhaa walijumuika kwenye msiba huo ambapo masuala ya kitaifa pia yalizungumziwa.