.
7th October, 2020
Chama cha Mawakili nchini LSK, kimesema kitaelekea bunge mnamo tarehe 12 mwezi huu, kupeleka notisi ya kuondoka kwa bunge la Taifa na Seneti, kwa kukosa kutimiza sheria ya thuluthi mbili ya uakilishi. Chama hicho kinasema baada ya zoezi hilo la jumatatu ijayo, bunge litakoma kuwa halali. Haya yanajiri baada ya jaji mkuu david maraga kutoa pendekezo la Bunge kuvunjwa kwa kutotekeleza sheria hiyo.