7th October, 2020
Baraza la ushauri wa usalama wa Kitaifa nchini limeelezea hofu yake kuhusiana na joto la kisiasa linaloendlea kupanda nchini. Baraza hilo linalosimamiwa na mkuu wa utumishi wa umma Dkt. Joseph Kinyua sasa limewaonya wanasiasa watakaochechea ghasia kuwa watachulikiwa hatua za kisheria. Kinyua anasema joto hilo la kisiasa linatishia usalama wa taifa na baraza hilo halitanyamaza kuruhusu hili kufanyika.