Wanjiku Kibe apoteza kiti cha Ubunge cha Gatundu Kaskazini, baada ya mahakama kuu kutoa uamuzi
07, Oct 2020
Wakazi wa eneo Bunge la Gatundu Kaskazini sasa watalazimika kurejea tena debeni kumchagua mbunge wao upya baada ya mahakama kuu kubatilisha uchaguzi wa mbunge wa sasa Wanjiku Kibe kwa misingi ya kukiuka sheria za uchaguzi. Haya yanajiri huku mpinzani wake aliyewasilisha kesi ya kupinga uchaguzi huo Clement Waibara akiridhishwa na uamuzi huo.