.
1st October, 2020
Serikali imesema walimu walioajiriwa na bodi simamizi za shule za umma ila hawana namba za usajili kutoka tume ya huduma za walimu, TSC, hawatalipwa. Waziri wa elimu profesa george magoha na katibu wa wizara, belio kipsang, wameiambia kamati ya elimu kwenye bunge la taifa kwamba sheria hairuhusu mwalimu ambaye hajasajiliwa na TSC kufunza kwenye shule za kenya.