.
30th September, 2020
Ubalozi wa uturiki nchini Kenya umeanza kusambaza vifaranga vya bure kwa kaunti 30. Kaunti ya Kakamega ikiwa ya kwanza kunufaika huku kila mkulima akipokea vifaranga 50 na vyakula katika mradi huo wa kuinua wakulima wadogo wadogo. Akizungumza katika hafla hiyo katibu mwandamazi katika wizara ya kilimo Lina Chebii amesema wizara yake na kaunti ya Kakamega imeanza mpango wa kujenga kichinjio cha kuku katika kaunti hiyo. Kaunti ya Kakamega pekee ina takriban kuku milioni 3.1