x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Vijana wengi wajihusisha na biashara ya pikipiki, hawajali usalama na kanuni za barabara

30, Sep 2020

Wahudumu wa bodaboda katika kaunti ya Busia wamelalamikia ongezeko la visa vya ajali barabarani zinazosababishwa na wanafunzi wa shule wanaodaiwa kujiingiza kwenye sekta ya uchukuzi msimu huu wa Korona. Wakizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa afisi mpya ya chama chao katika eneo la Ojamii eneo bunge la Teso kusini kaunti ya Busia, wahudumu hao wamesema kuwa wanafunzi wamesajili idadi kubwa ya ajali zinazohusiana na pikipiki kwani wengi wao wanaziendesha bila kuzingatia sheria za barabarani.  Kupitia kwa viongozi wao,wahudumu hao wamesema kuwa zaidi ya wanafunzi mia moja wanauguza majeraha ya mwili baada ya kuhusika kwenye ajali za barabarani tangu shule zifungwe mwezi machi mwaka huu,huku wakitaka vitengo husika kuingilia kati na kuwachukulia hatua kali wanaojihusisha. 

Feedback