30th September, 2020
Wafanyakazi wa maduka ya Tuskys waliandamana kulalamikia kutolipwa kwa mishahara yao ya miezi mitatu. Maandamano hayo yamekuwa msumari moto kwenye kidonda ikizingatiwa kwamba tusky’s imejipata katika hali ngumu ya kifedha, biashara nyingi zikiitaka kampuni hiyo kuwalipa madeni yao.