24th September, 2020
Mahakama kuu imesimamisha utekelezwaji wa ushauri wa jajai mkuu kwa rais kuwa bunge livunjwe. Kwenye uamuzi wake jaji Weldon Korir amesema kwamba kesi iliyowasilishwa na Leina Konchella na Mohsen Abdul Munasar kupinga ushauri huo wa jaji mkuu, imegusia masuala muhimu ya vipengee vya sheria. Jaji korir ameamuru kuwa kesi hiyo isikizwe na majaji wasiopungua watatu, watakaoteuliwa na yuyo huyo jaji mkuu. Awali chama cha wanasheria nchini LSK kilitoa makataa kwa rais kuvunja bunge kufikia oktoba 12 la sivyo kiandae maandamano ya wananchi hadi bungeni. Huyu hapa Nelson Havi, rais wa LSK.