×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Wizara ya afya kuhusu Korona nchini, Je, shule ziko salama kwa Korona?

23rd September, 2020

Kwa muda sasa, Taifa limekuwa na visa vichache kuripotiwa vya Covid19, jambo ambalo limiechochea wizara ya afya kusema kuwa shule zitafunguliwa wakati wowote. Japo shirika la afya ulimwenguni (WHO) limeonya kuwa janga hili halitakwisha hivi karibuni, usalama wa wanafunzi umetiliwa shaka pindi tu shule zitakapofunguliwa.

 

Wizara ya Afya sasa inasema mpango wa kufungua shule nchini mwezi ujao, utawapa wanafunzi nafasi ya kujizoesha na mandhari mpya ya shule, kabla ya masomo kung’oa nanga kikamilifu. Haya yanajiri baada ya wizara ya elimu kutangaza kwamba zaidi ya wanafunzi milioni 15 watarejea darasani mwezi ujao, ila chini ya kanuni za kupambana na jinamizi la Korona.

.
RELATED VIDEOS