Jubilee yampiga Ruto chenga, chama hakitakuwa na mgombea kwenye uchaguzi wa eneo Bunge la Msambweni
23, Sep 2020
Naibu Rais William Ruto amesema huenda akawa na mgombea wa kumuunga mkono kwenye uchaguzi mdogo wa eneo Bunge la Msambweni. Hii ni licha ya kuwa Chama cha Jubilee kupitia Katibu Mkuu Raphael Tuju kutangaza kuwa hakitawasilisha mgombea katika kinyang’anyiro.