18th September, 2020
Mwenyekiti wa baraza la magavana wycliffe oparanya Amewataka magavana kuhakikisha kaunti zimerejelea Shughuli zake mara moja baada ya kaunti mbali mbali Kusitisha huduma zake kutokana na vuta ni kuvute katika Bunge la seneti. oparanya na Magavana wengine wameshabikia hatua ya bunge la seneti Kupitisha mfumo mpya wa ugavi wa fedha za kaunti. Wakati Huo huo magavana wakitakiwa kutumia fedha hizo kuleta Maendeleo katika kaunti zao. Viongozi mbali mbali Walizungumza katika hafla ya kuorodhesha na kutathmini miradi Aliyotekeleza gavana wa bungoma wycliffe wangamati Katika chuo kikuu cha kibabii