Peter Imwatok atetea NMS, asema imeleta maendeleo Nairobi
16, Sep 2020
Kiranja wa wachache katika Bunge la Kaunti ya Nairobi, Peter Imwatok, ameitetea mamlaka ya huduma za jiji la Nairobi, NMS, na kulitaka bunge la Kaunti ya Nairobi kupitisha sheria zifaazo ili kurahisisha utendakazi wake. Kwenye kikao na wanahabari, Imwatok ametaja maedndeleo yaliyotekelezwa na mamlaka hiyo katika kipindi cha miezi mitano pekee kuwa ithibati kamili ya ufanisi wake.