16th September, 2020
Serikali imeondoa hofu ya biashara kubomolewa na wawekezaji kufurushwa kutoka eneo Lunar Park hapa Nairobi, kwa kusudi la ujenzi wa mradi wa maegesho au stendi ya magari ya abiria. Ingawa taarifa za awali ziliashiria kwamba ardhi hiyo ilidhamiriwa ujenzi wa barabara ya juu kwa juu ya kuunganisha jiji la Nairobi na uwanja wa ndege wa Jkia, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya huduma za jiji la Nairobi na viunga vyake, Meja Jenerali Mohamed Badi, amefafanua kwamba ardhi hiyo imekabidhiwa mamlaka hiyo kwa madhumuni ya ujenzi wa maegesho ya magari.